VYUMA VYAKAZA REAL, CITY, ARSENAL NA BAYERN MUNICH

Klabu ya Arsenal inayoongozwa na kocha mikel Arteta kule uingereza imelazimishwa sare ya bao 2-2 dhidi ya klabu ya Bayern Munich ya kule ujerumani katika mechi ya raundi ya kwanza ya kombe la klabu bingwa barani ulaya hatua ya robo fainali.

Ni mechi ambayo ilikuwa imejaa mbwembwe za mashabiki wa Gunners wakiwa nyumbani pale Emirates hasa kwa matumaini ya kuandikisha matokeo bora.

Arsenal wamepata mabao yao mawili kupitia kinda Bukayo Saka pamoja na Leandro Trossard huku Bayern Munich wakipata mabao yao kupitia Serge Gnabry ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ya Arsenal huku bao la pili la wajerumani hao likiwekwa kimyani na Harry Kane kupitia mkwaju wa Penalti.

Kwa upande mwengine Manchetser City wameilazimisha Real Madrid sare ya mabao 3-3. City inayoongozwa na kocha Pep Guardiola imepata mabao yake kupitia Bernado Silver, Phil Foden lakini pia Josko Gvadiol huku Real wakipata bao lao la kwanza pale Rodri alipojifunga kwa kupinda mpira wa Eduardo Camavinga, Rodrigo akifunga bao la pili na Federico Velverde akifunga bao la tatu.

Sasa Real wamejisababishia kibarua kigumu watakaposafiri ugenini Etihad katika mechi ya marudiano tarehe 17 mwezi huu.