VILABU VYOTE VICHEZE MAGARINI, FKF MAGARINI YASEMA

Katibu wa shirikisho la soka la eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Emmanuel Kazungu amethibitisha kuwa vilabu vyote vya magarini ambavyo kwa miaka ya nyuma vimekuwa vikishiriki katika ligi ya eneo bunge la Malindi sasa ni sharti vitashiriki ligi ya Magarini huku usajili ukiwa unaendelea.

Kulingana na Emmanuel ni kuwa vilabu vinavyolengwa hasa ni kama vile Sandoki FC, Silver Pentagon pamoja na Sabaki City ambavyo awali vilikwamilia ligi ya Malindi kwa muda.

Kupitia mazungumzo ya njia ya simu Emmanuel ameeleza umuhimu wa vilabu hivyo kushiriki katika ligi ya Magarini akihoji kuwa wakati mwengine vilabu hufungiwa mashindano kisa kukosa ushirika na fkf ya tawi husika.

Ligi ya Magarini msimu huu itakuwa na vyungu takribani vinne au hata zaidi kama vile Gongoni, Magarini, Adu, Marafa na labda Sabaki na kwengineko na tayari mikakati ya kutafuta wadhamini wa ligi hiyo yanaendelea ikizingatiwa kuwa msimu huu ada ya usajili kwenye ligi iko chini na haiwezi toa zawadi mwisho wa msimu.