Mkurugenzi wa KWS kaunti ya Kwale Jocob Orale amesema wanaendeleza mikakati ambayo itasaidia kudhibiti visa vya ukataji miti kiholela na uwindaji haramu katika msitu wa Shimba Hills.
Orale amesema wameweka uzio upya ambao unazunguka mbuga hiyo ili kudhibiti visa hivyo.
Kulingana na Orale visa vya uwindaji haramu vimekuwa vikiathiri sekta ya utalii nchini kwani idadi ya wanyamapori huwa inapaungua mbugani.
Kwenye kikao na waandishi wa habari Orale amethibitisha kuwa visa vya uwindaji haramu katika Mbuga hiyo ya Shimba Hills vimepungua kwa kiwango kikubwa vikilinganishwa na vya miaka ya nyuma.
VISA VYA UWINDAJI HARAMU VIMEPUNGUA KATIKA KAUNTI YA KWALE

