MIRAJJ ABDILLAHI AWAHIMIZA VIONGOZI WA PWANI KUIPA ELIMU KIPAUMBELE

Seneta mteule Miraj Abdillahi ametoa wito kwa viongozi wa kanda ya pwani kuipa elimu kipaumbele.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Miraj amesema ni lazima kuwe na mikakati ambayo itawekwa na viongozi, wadau mbalimbali pamoja na serikali katika kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika kanda ya pwani.
Miraj amesema ili viwango vya elimu viimarike kanda ya pwani ni lazima hayo yatekelezwe kwani pia yatasaidia katika kudhibiti hali ya umasikini na visa vya uhalifu ambavyo vinatekelezwa na vijana walio na umri mdogo.
Kauli yake imeungwa mkoni na Juma Athman Lubambo ambaye ni katibu mkuu wa muungano wa shule za mabanda nchini APBET na kusema idadi kubwa ya wanafunzi kutoka familia zisizojiweza kifedha kanda ya pwani hawajaweza kujiunga na shule za upili licha ya kufanya vyema kwenye mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka jana wa 2022.