Mkufunzi mkuu wa klabu ya Kibra United Ray Omondi anasema kwamba ligi ya daraja la kwanza kitaifa inakosa mashiko na ushindani kutokana na kwamba wachezaji katika ligi hiyo kucheza wakiwa na tamaaya malipo baada ya mechi kuliko kuonyesha kukua kwa viwango vyao.
Mkufunzi huyo anahoji kwamba ligi ya daraja la pili ndio ligi yenye ushindani zaidi pamoja na vijana kuonyesha vipaji vyao uwanjani.
Omondi anadai kwamba tama ya hela miongoni mwa wakuu wa vilabu ndio jambo ambalo linaregesha nyuma viwango vya mchezo katika ligi ya daraja la kwanza.

