VIONGOZI WA NYANZA WAMSIFIA KALONZO MUSYOKA

Viongozi wa Nyanza wamemsifia kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa kusimama kwa muda mrefu na kinara wa ODM, Raila Odinga.
Wakiongozwa na gavana wa Siaya James Orengo viongozi hao wamemsifia Kalonzo kwa ukakamavu wake katika kuamini uongozi wa Raila licha ya kupokea pingamizi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa ukambani ambao hawakutaka Kalonzo amuunge mkono Raila.
Ni kauli iliyoungwa mkono na seneta wa Siaya, Oburu Odinga ambaye pia amemshukuru Kalonzo kwa kutoyumbishwa katika kufanya maamuzi ya kumuunga mkono Raila.
Wakati uo huo, Oburu ameonyesha kutoridhishwa na hatua ya serikali kumrejesha Miguna Miguna humu nchini huku pia akisema kuwa hakuna mageuzi yoyote atakayoleta Miguna kwenye eneo la nyanza kama alivyodai siku ya ujio wake.