GAVANA WA KILIFI ASEMA SERIKALI YAKE HAIJAWEZA KUWASILISHA BAJETI YA ZIADA

Serikali ya kaunti ya Kilifi imetakiwa kushughulikia swala la ukame, kwa kuweka mikakati ya kutosha ili kuhakikisha wakaazi wanapewa msaada wa kutosha na kuzuia maafa katika maeneo yaliyoathirika zaidi.
Hii ni baada ya gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mungaro, kueleza kuwa serikali yake haijaweza kuwasilisha bajeti ya ziada, katika bunge la kaunti kwani bado haja kamilisha masuala ya uteuzi wa viongozi, watakao shikilia nyadhifa mbalimbali kwenye serikali hiyo.
Mung’aro amesema kuwa huenda bajeti hiyo ikachukua muda zaidi, kabla ya kuwasilishwa bungeni kwani hadi kufikia sasa, bado bunge hilo liko katika awamu ya kuunda kamati zake, zitakozo saidia katika kushughulikia masuala mbalimbali kwenye serikali ya kaunti.
Aidha Mwakilishi wadi wa Sokoke Harrison Thaura Mweni, amepinga kauli hiyo na badala yake kuwawataka viongozi kufanya majukumu yao ipasavyo, hususan wakati huu ambapo mwananchi anahitaji msaada wa dharura.