Vilabu vya soka mashinani vinazidi kulilia hali ngumu ya kuendesha michezo kutokana na ukosefu wa ufadhili licha ya kuwepo kwa serikali za ugatuzi.
Mkufunzi wa klabu ya Yanga FC iliyoko mjini malindi mwite Collins Omol ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kuja mashinani na kusaidia kusuluhisha hali ngumu ya kuendesha michezo wanayopitia kwa sasa.
Amemtaka afisa mkuu wa michezo kaunti ya Kilifi Naftali Owino kuja mashinani na kuokoa timu za mashinani kwa angalau kuzipiga jeki na usafiri kupitia serikali iliyoko madarakani kwa sasa ili kuleta afueni katika kuendesha michezo.
”Naftali tunajua hata yeye ni mchezaji. Na hata ashawahi kuchezea timu ya Yanga wakati fulani na bila shaka anaelewa changamoto za wachezaji huku mashinani. Sisi tunamuomba aje mashinani atuokoe kupitia serikali ya kaunti angalau tupate usafiri. Lile basi tulilonunuliwa na mama Aisha saa hii limekufana tunapitia kipindi kigumu katika usafiri.” Alisema Omol.

