HATIMAYE YOUNG BULLS YATOLEWA KILELENI

Klabu ya Rainbow fc kutoka kaunti ya Nairobi sasa imekwea kileleni mwa jedwali la ligi ya daraja la kwanza kitaifa baada ya wikendi hii kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Dandora Youth katika uwanja wa ugenini.

Rainbow sasa imeishukisha Young Bulls kileleni kwa utofauti wa mabao baada ya Young Bulls kutoka pwani kuongoza ligi hiyo kwa kipindi kirefu msimu huu. Wote wako na alama sawa, alama 61.

Kwengine Malindi Progressive wanazidi kulemewa kwenye ligi kwani wamezidi kuandikisha matokeo mabaya katika mechi za hivi punde. Wikendi ilopita Malindi Progressive walitandikwa kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Administration Police.

Liberty Sports academy walipiga sare tasa dhidi ya Nairobi United wakati Equity nayo ikipiga sare ya bao 1-1 dhidi ya Kibra United huku vijana wa Isiolo Olympic Pirates wakisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya 3K FC.