Jumla ya vijana watano ambao wanadaiwa kutekeleza visa vya wizi wa kimabavu katika mitaa ya wadi ya Shella na mji wa Malindi kaunti ya Kilifi wametiwa mbaroni.
Haya ni kwa mujibu wa naibu chifu wa eneo hilo la Shella Nicodemus Mwayele ambaye amesema idara ya usalama imekuwa ikiendeleza msako dhidi ya magenje ya kihalifu katika eneo hilo hatua ambayo imetokana na ongezeko la visa vya watu kuvamiwa na kuporwa mali zao katika eneo hilo.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake naibu chifu huyo amesema vijana hao ambao walianza kukamtwa mapema wiki hii ni wa kati ya umri wa miaka 20 – 24 na ni wakaazi wa eneo la Muyeye katika wadi hiyo ya shella.
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao wamewahi kuvamiwa na makundi hayo wakiongozwa na Festus Isaac, William Katana na Samuel Kitsao wamelalamikia utovu wa usalama katika eneo hilo na kusema ipo haja ya idara usalama kuendelea kuwachukulia hatua wale wanaotekeleza visa hivyo eneo hilo.
VIJANA WATANO WANOJIHUSISHA NA UHALIFU ENEO LA SHELLA MJINI MALINDI WATIWA MBARONI

