Idadi ya vifo vya Watoto kabla ya kuzaliwa na hata baada ya kuzaliwa katika kaunti ya Kilifi vimeripotiwa kupungua kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Haya ni kulingana na ripoti ya utafiti wa serikali kuu kupitia idara ya afya nchini ambayo imebainisha kupungua kwa visa hivyo kutokana na juhudi za akina mama hao Kwenda kliniki na pia kujifungua hospitalini.
Mshirikishi wa afya ya uzazi na jinsia kwa vijana kaunti ya Kilifi Kenneth Miriti amesema mafanikio hayo pia yametokana na akina mama wengi kupata huduma hizo kupitia Linda mama ambayo inagharamia mahitaji yao ya kifedha, mafunzo kutoka kwa wahudumu wa afya ya nyanjani na pia kupitia ushirikiano mwema ulioko baina ya kina mama hao na wahudumu wa afya katika vituo vya afya.
Kwa upande wake Waziri wa afya kaunti ya Kilifi Peter Mwarogo serikali ya kaunti ya Kilifi kupitia idara ya afya kauntiya Kilifi watawasilisha mswada bungeni hivi karibuni unaolenga kuwajumuisha wafanyikazi wa afya ya nyanjani Pamoja na wahudumu wa afya kaunti ya Kilifi ili kuweza kupokea fedha zitakazowasaidia katika kutekeleza majukumu yao ili kutoa huduma bora Zaidi.
RIPOTI YA WIZARA YA AFYA YAONYESHA IDADI YA VIFO VYA WATOTO KABLA YA KUZALIWA NA BAADA YA KUZALIWA VIMEPUNGUA KILIFI

