Victor Mugubi Wanyama nahodha wa zamani wa kikosi cha Harambee Stars ya Kenya alicheza mechi yake ya mwisho na kikosi chake cha sasa cha Montreal kunako mitanange ya major soccer league na kupoteza kwa mabao 3-1 kwenye mechi hiyo ya semi fainali dhidi ya mabingwa watetezi New York City Fc usiku wa kuamkia leo.
Wanyama alitangaza mapema mwezi huu kwamba atakuwa anaihama klabu hiyo baada ya kuwepo hapo kwa miaka miwili baada ya kutoka Toteham Hotspurs ya ligi kuu nchini uingereza na sasa tetesi zasema kwamba huenda akaibukia LA Galaxy ya marekani kwa mkataba mwengine wa hela ndefu kweli kweli.
Ikumbukwe kwamba akiwa Montreal Wanyama amekataa katakata kusaini kuongeza mkataba baada ya kupewa offer na waajiri wake na tayari alikuwa anatia mfukoni milioni 289.9 kwa mwaka.

