Vilabu vya mashinani vya soka vinazidi kujitayarisha kwa msimu mpya wa mwaka 2022/2023 na mechi za kirafiki zinazidi kurindimwa. Wikendi hii vijana wa Pwani Fc waisafiri hadi mjini malindi kuvaana na Furunzi fc inaoongozwa na mkufunzi Nero Chishenga mtanange ilotamatika kwa sare ya bao 1-1.
Katika uwanja wa Prison eneo bunge la malindi kaunti ya kilifi mtanange mzito wa kirafiki ulishuhudia vijana wa Bosuster ya Bomani wakitandikwa kichapo cha mabao 2-0 na Zamakec.
Akizungumza na Tama la Spoti mkufunzi wa Zamakec Micheal Jeffah alisema kwamba amefurahishwa na kiwango cha vijana wake kwa kutwaa ushindi huo nyumbani akisema sasa wanahitayarisha kwa mashindano ya mini league ya County ambayo huenda yakafanyika hivi punde.
Hata hivyo amewapongeza Bosuster kwa kurudi kwenye anga za soka za mashinani eneo bunge la magharini akisema kwamba vijana hao licha ya kupoteza mechi yao ya wikendi hii lakini waionyesha kiwango cha juu.

