UHISPANIA YATINGA FAINALI

Timu ya taifa ya Uhispania kwa upande wa kinadada imefuzu kutinga fainali za mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea katika mataifa ya Australia pamoja na New Zealand.

Uhispania wamefanya hivyo baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya kinadada ya Sweden mtanangwe ambao umechezwa adhuhuri ya leo 15- Julai 2023

Sasa timu ya taifa ya Uhispania itakuwa inamenyana mshindi wa kati ya Australia na Uingereza wawili hao watakapokuwa wanakutana kesho.

Sweden watavaana na atakayepoteza kati ya wawili hao katika kung’ang’ania nafasi ya tatu na wanne.

Mechi kati ya Australia na Uingereza itachezwa kesho saa saba mchana katika uwanja wa Olympic ulioko jijini Sydney Australia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *