Mkufunzi mkuu wa klabu ya Tusker FC Robert Matano anasema anaimani kubwa kwamba licha ya juhudi za kutetea ubingwa wa ligi kuu ya fkf vijana wake watamaliza katika nafasi nzuri msimu huu.
Fundi huyo wa soka amesema kwamba kwa sasa vijana wake wako imara licha ya majeraha yaliyokuwepo, majeraha ambayo yaliwaponza mwanzo wa msimu.
Hadi sasa wanamvinyo Tusker wamesajili ushindi mara tatu mfululizo ushindi ambao ni pamoja na ule wa jana wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Bandari fc kutoka pwani ya Mombasa.

