Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Erik ten Hag amemtetea kiungo wa kati wa kikosi chake Bruno Fernandes baada ya kukosolewa vikali mitandaoni na baadhi ya wachambuzi wa soka na mashabiki kutokana vitendo vya hasira alivyoonyesha kwenye pambano walilopoteza dhidi ya Liverpool kwa mabao 7-0 siku ya Jumapili.
Bruno Fernandes alionyesha hasira baada ya kumsukuma msaidizi wa refarii kwenye dakika ya 81 ya mchezo na kufuatia tukio hilo kumekuwa na shinikizo la kumpokonya bandi ya unahodha kiungo huyo raia wa ureno na Ten Hag amemtetea na kumtaja Bruno kama mchezaji mwenye msukumo na mchango mkubwa klabuni humo.
Baadhi ya wachambuzi wa soka wakiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United Garry Neville pamoja na Chris Sutton ni kati ya wale waliokashifu vitendo vya Bruno wakisema wapo wachezaji bora zaidi kwenye kikosi cha Manchester United wenye uwezo wa kuwa nahodha wa timu hiyo.

