Sajili mpya ya Slavia Praha kutokea Czech Republic Timothy Ouma maarufu kama Babu, anapania kuzifuata nyayo za mshambualiaji wa zamani wa Inter milan Mc Donald Mariga, akiwa na ndoto ya kushinda kombe la Klabu Bingwa Ulaya .
Sawia na Upande wake wa Zamani Elfsborg ya kule Uswidi, Praha pia imebanduliwa nje ya michuano ya kombe la Bara Europa ikimaliza katika nafasi ya thelathini na alama tano pekee.
Kwa sasa Praha imeweka hai matumaini yao ya kushinda ligi kuu ya nchini humo baada ya miaka mitatu, wakifungua mwanya wa alama kumi kileleni na alama hamsini na tatu baada ya mechi ishirini.
Ouma alitangazwa rasmi kuwa mali ya Slavia Praha siku ya Jumapili, baada ya kusaini mkataba wa milioni mia nne sabini na tatu pesa Taslim Za Kenya.

