SHIMANZI FC NA ZIWANI YOUTH TUTAMBAMBANA KISHERIA – COLLINS OMOL

Meneja wa klabu ya Yanga FC Collins Omol klabu inayoshiriki ligi ya daraja la nne kitaifa  la fkf kutoka Malindi kaunti ya Kilifi amekanusha madai ya vilabu vya Shimanzi na Ziwani Youth kuwa mechi ambazo hawakucheza na Yanga watapewa alama za bwerere kwa sababu klabu hiyo ilishindwa kuheshimu ratiba.

Kulinga na  Omol ambaye amezungumza na Tama L a Spoti ni kuwa kesi hizo kwa sasa ziko mikononi mwa fkf na sasa sio muda wa kulumbana na wapinzani wao akidai kuwa shirikihso liko na sheria zake kuhusu masuala kama hayo.

”Walk Over iko na vipengele vyake, katika hiyo mechi kila kitu kilizingatiwa? Sio kila jambo wapinzani wetu walizingatia. Kukosa ufahamu wa sheria za fkf ndio unawambia kuwa mechi hiyo sisi hatukuheshimu ratiba. Hizi sheria za kuheshimu ratiba sio za kenya hata ulaya zipo. Juzi Gor Mahia walichelewa kwa mechi na kisha mechi ikachezwa. Sisi Yanga je?” Alisema Collins

Collins ameongeza kuwa wanaendelea na mechi zao za msimu huu wakisubiri siku ya kusikilizwa kwa kesi zao na shirikihso la fkf

”FKF iko na wakati wake wa kusikiliza kesi na kila mwenye jambo atapigia simu kuna siku zake za kesi hizo kutatuliwa. Kwa sasa sisi tunaendelea na mechi zetu ila tutapambana mwisho wa msimu tubaini ukweli kutoka kwa shirikisho.”  Aliongeza Collins.