Mabingwa Watetezi wa Ligi kuu hapa Nchini Gor Mahia, wamemtangaza Sinisa Mihic kama Mkufunzi wao mpya akivivaa viatu vya Zedekiah Zico Otieno, aliyekua akihudumu kama mKufunzi wa Muda tangu Novemba mwaka Jana Leonardo Neiva Alipotimuliwa.
Mihic ana uzoefu wa kufanya kazi barani Africa, akiwahi kua mkufunzi msaidizi katika klabu ya Al Merrikh huko Sudan mwaka wa Elfu Mbili na Tisa, na mwaka mmoja baadae kufanya kazi katika klabu ya Al Nasr huko Libya.
Baada ya Kupata ushindi wa Magoli mawili kwa Moja dhidi ya Posta Rangers hapo jana, Nguli Huyo atakua na kibarua kizito dhidi ya wanamvinyo Tusker siku ya Jumamosi Huko Machakos, zico akirudia majukumu yake kama naibu mkufunzi

