SHEKHUNA ABBAS AWAONYA WATOTO WANAORANDARANDA OVYO KISIWANI AMU

Mwakilishi wa wadi ya Mkomani kaunti ya Lamu Shekhuna Abbas amewaonywa wanafunzi kisiwani Amu dhidi ya kuzurura ovyo nyakati za usiku.
Akizungumza katika kaunti hiyo Abbas amewataka kusalia majumbaNI na kuendela kusoma ili wafanye vyema kwenye masomo yao na kusema watakaopatikana wakirandaranda kisiwani humo watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, amewahimiza wazazi kuhakikisha wanajukumika vilivyo katika kuhakikisha wanasoma wanapokuwa nyumbani ili kuwadhibiti dhidi ya kushawishika kujiunga na magenge ya kihalifu.
Amesema iwapo wazazi watawajibika watoto wengi kisiwani Amu wataepukana na utumiza wa dawa za kulevya.