KAMISHNA WA TAITA TAVETA KUANDAA MAZUNGUMZO NA IDARA YA KWS

Kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Loyford Kibara amesema idara ya usalama kwenye kaunti hiyo itafanya mazungumzo na ile ya KWS ili kuwanusuru mifugo wa wenyeji msimu huu wa kiangazi.
Amesema wanapania hivi karibuni kufanya mazungumzo hayo na mkurugenzi mkuu wa KWS ili kuona kuwa wafugaji katika kaunti hiyo wanaruhusiwa kulisha mbugani.
Kamishna huyo amesema kiangazi ambacho kinaendelea kushuhudiwa katika kaunti hiyo na nchini kote kinaendelea kuwaathiri mifugo wengi.