Serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kujenga kiwanja cha kimataifa kama njia moja ya kuwezesha talanta na michezo mashinani.
Naibu gavana wa kaunti hii Florence Chibule akiwa katika mahojiano na mwanahabari wetu hapa Lulu Fm amethibitisha kwamba serikali inayoongozwa na gavana Gideon Maitha Mungaro inalenga kuanza mradi wa ujenzi wa kiwanja cha kisasa kama njia moja ya kukuza michezo pamoja na talanta mbalimbali za vijana mashinani.
Hata hivyo Chibule amewapongeza wawakilishi wadi wa wadi mbalimbali za kaunti ya Kilifi kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha michezo kwa kuanzisha mashindano mbalimbali mashinani kama njia moja ya kukuza talanta za vijana lakini pia kuwawezesha na vifaa vya michezo.

