FERNANDO SANTOS APATA KAZI POLAND

Ni rasmi sasa mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno ya wanaume katika soka  Fernando Santos amepewa kibarua cha kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Poland.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 68 anamrithi Czesław Michniewicz aliyefutwa kazi baada ya kutolewa katika mashindano ya kombe la dunia katika hatua ya raundi ya 16 bora.

Santos mwishoni mwa mwaka jana alijiuzulu kutoka timu ya taifa ya Ureno baada ya kupoteza kwa Morocco katika mechi ya robo fainali.