SENETA MOHAMED FAKI AWATAKA WAKENYA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE MAANDAMANO YA LEO

Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohamed Faki amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi hii leo kwenye maandamano yanayoongozwa na azimio la umoja one Kenya kuishinikiza serikali kuu kuwajibikia changamoto zinazowakabili wananchi.
Faki amesema hali ya kupanda kwa gharama ya maisha, kunaendelea kuwaathiri Wakenya wengi na ni lazima serikali kuu iwajibishwe ili kuwanusuru.
Akizungumza akiwa kwenye kaunti ya Mombasa, Faki amekosoa hatua ya Rais William Samoei Ruto, kuondoa ruzuku kwenye bidhaa muhimu kama vyakula na petroli na kusema hatua hiyo imesababisha kupanda maradufu kwa bei za bidhaa hizo nchini..
Wakati huohuo amewataka maafisa wa usalama, kutovuruga maandamano hayo ya Jumatatu kwani yatakuwa ya amani.