FIKIRINI JACOBS ATEULIWA NA SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI

Kiongozi wa vijana katika chama cha ODM kaunti ya Kilifi, Fikirini Jacobs ameteuliwa na serikali ya kaunti ya Kilifi, katika nafasi ya mkurugenzi wa kitengo cha kuangazia utekelezwaji wa miradi ya serikali ya kaunti hii ya Kilifi.
Akizungumza wakati uteuzi huo gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro amesema kuwa bado wataendeleza uteuzi wa viongozi katika nafasi mbali mbali, ili kuboresha utendakazi wa serikali yake.
Vile vile gavana huyo pia amemteua kasisi Tom Dawa wa dhehebu la kianglikana, kuchukua nafasi ya afisa wa kutathmini shughuli za serikali ya kaunti ya Kilifi, ikiwemo miradi mbali mbali ya serikali.
Wakati uo huo amesema kuwa tayari amekabidhi bunge la kaunti hii ya Kilifi, majina kamati ya kutekeleza uteuzi wa makamishna, wa tume ya kuajiri wafanyakazi wa serikali ya kaunti, pamoja na katibu mkuu wa serikali ya kaunti ya Kilifi.