MUUNGANO WA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI WAMTAKA RAIS RUTO KUFANYA MASHAURIANO NA RAILA ODINGA

Muungano wa maaskofu wa kanisa katoliki sasa unamtaka Rais William Ruto na Kiongozi wa Azimio Raila Odinga kufanya mashauriano na kuzima tofauti za kisiasa humu nchini.
Askofu Philip Anyolu ambaye ni askofu mkuu wa jimbo la Nairobi anasema kuwa joto la kisiasa lililopo nchini linahatarisha amani na kuibua taharuki katika maeneo mengi nchini.
Wakati huo huo, Muungano wa maendeleo ya wanawake nchini pia kinamtaka rais Ruto na Raila kuanzisha mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kudumu.
Haya yamejiri huku hirika la ndege la Kenya airways limetangaza kufunga ofisi zake kwa muda kwenye maeneo ya kuuza tiketi mjini Kisumu sawia na Johanesburg taifa la afrika kusini kufuatia maandamano yanayotarajiwa hii leo mtawalia.
Maandamano sambamba na ya leo humu nchini yatakuwa yakifanyika pia Johanesburg yakiongozwa na chama cha Economic freedom fighters, EFF ambacho kinampinga rais Cyril Ramaphosa kikiongozwa na Julius Malema.