Mkufunzi wa klabu ya AFC Leopards mwite Patrick Aussems anasema kwamba msimu huu matumaini yao ya kushinda ubingwa wa ligi kuu ya fkf primia league yamepotea ila watajitahidi kuandikisha matokeo mazuri dhidi ya Gor Mahia wikendi hii.
mechi hiyo ambayo ni daby ya mahasimu hawa wa jadi itachezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Nyayo na itapeperushwa moja kwa moja na televisheni ya kigeni kutoka taifa jirani la Tanzania Azam TV baada ya makubaliano ya shirikisho na kituo hicho cha habari.
Mkufunzi Aussems anasema Ingwe watapambana kufa kupona katika mechi hiyo na wanaichukulia kama fainali lakini pia kudumisha heshima yao katika dabi hii na kuchukua alama tatu. Kwa sasa Ausseems anazidi kunoa kikosi chake kwa mechi za ligi zilizosalia ili kumaliza msimu huu katika nafasi nzuri.

