SANGO SPORTIFF YAZIDI KUBOREKA

Mkufunzi wa klabu ya Sango Sportiff  inayoshiriki ligi ya Divisheni ya Pili Coach Rigo, ameelezea kwamba  kurekebisha makaosa  waliyofanya kwenye mechi yao Iliyopita, Ndio Kulichangia Ushindi wao Mnono Dhidi ya Mariakani Fc, akiusifia Mchezo Mzuri ulioonyeshwa na Upande huo wa Mkufunzi Hassan Seif.

Sportiff waliicharaza Mariakani magoli Manne bila jawabu kwao nyumbani, Timu Hio sasa Ikishikilia nafasi ya Pili na alama Ishirini na Tisa baada ya Mechi Kumi ni Mbili, Kukiwa na Utofauti wa mechi nne na alama tisa Kati yao na  vinara wa Ligi Simba Apparel.

Aidha Coach Rigo ameongezea kwa Kusema Ya kwamba wanajitayarisha Vilivyo Kuwakabili Sparki Youth, azimio Lao Likiwa Lilee la kuvuna Alama Tatu, mechi Hio ikiratibiwa Kupigwa Siku ya Jumapili tarehe mbili ugani Santiago Itsowe.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *