Raisi wa Shirikisho la Soka Hapa Nchini Hussein Mohammed, Ameelezea Mipango Kabambe waliyoieka kama Shirikisho Kuhakikisha ya Kwamba timu ya Taifa Ya wachezaji Wasiozidi umri wa Miaka Ishirini, wanajitayarisha Viliovyo Kuelekea kwenye Mashindano ya AFCON Aprili mwaka Huu Huko Ivory Coast.
Mipango Hiyo iliyowekwa na FKF Ni kuhakikisha kwamba Uchaguzi wa Wachezaji Unafanywa Vizuri, Ukijumuisha Wachezaji Kutoka pande zote za Nchi, pamoja Na Kuhakikisha kwamba Kikosi Hicho kina Pata Muda mwafaka kambini wa Kufanya mazoezi ya Kutosha.
Kufuatia Droo Iliyofanywa terehe kumi na tatu February mwaka Huu Huko Misri, Rising Stars walipangwa Kwenye Kundi C Pamoja Na Bingwa Mtetezi Senegal, washindi wa Zamani Zambia na Sierra Leone Wanaokua Kwa Kasi.

