RONALDO KUFANYA KIKAO NA ERICK TEN HAG KABLA KUONDOKA OLD TRAFFORD

Mshindi mara tano wa taji la Ballon D’or Cristiano Ronaldo anatarajiwa kufanya kikao chengine cha mazungumzo magumu na Erik ten Hag, huku taarifa zikisambaa kuwa Manchester United itamruhusu fowadi huyo kuondoka kwenye dirisha la usajili la Januari.

Mustakabali wa Ronaldo bado haujulikani baada ya Ten Hag kumtimua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kutokana na kitendo chake cha kujiondoa uwanjani kabla ya mechi kumalizika United ilipomenyana na Tottenham dimbani Old Trafford baada ya kukataa kuingia kama mchezaji wa akiba wakati wa ushindi wao wa 2-0 dhidi ya vijana wa Antonio Conte Jumatano wiki jana.

Ronaldo yuko chini ya kandarasi hadi mwisho wa msimu huu na Ten Hag ameweka wazi kuwa anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 akamilishe mkataba wake katika klabu hiyo.

Hata hivyo, uongozi wa United unaripotiwa utamruhusu Ronaldo kuondoka wakati wa uhamisho wa Januari kutokana na uhusiano wake na Ten Hag