KAMATI YA KUKABILIANA NA UKAME KWAUNTI YA KWALE YAWEKA MIKAKATI THABITI

Kamati ya kukabiliana na ukame kaunti ya Kwale imeweka mikakati ya kudhibiti visa vya wizi wa chakuka cha msaada kwa wenyeji ambao wameathirika na baa la njaa.
Haya ni kulingana na naibu Kamishna wa eneo bunge la Matuga Lucy Ndemo ambaye amesema ni lazima walengwa wapate chakula chao cha msaada kama inavyopaswa kulingana na taratibu zilizowekwa.
Naibu kamishna huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo katika eneo bunge la Matuga ametoa onyo kwa watakaojaribu kuiba chakula hicho cha msaada na kusema watakaopatikana watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha, amesema chakula hicho cha msaada kitatolewa kwa wanafunzi wanaokabiliwa na baa la njaa kwenye shule za kutwa na zile maalum ili waweze kuendeleza masomo yao bila changamoto zozote.