RAGA YA SHULE ZA UPILI MALINDI YAIMARIKA

Viwango vya raga katika eneo bunge la Malindi vimeanza kukua tofauti na miaka ya nyuma hasa michezo inayoshirikihswa mashuleni.

Hiyo ni kulingana na wasimamizi wa michezo ya shule za upili katika eneo hili ambao wamethibitisha kuwa Malindi imeandikisha historia ya kuhusisha raga ya kinadada ya wachezaji saba kila upande kwa mara ya kwanza kabisa.

Akizungumza na Tama la Spoti, Huluma Arnest ambaye ni kocha wa raga katika eneo hili kutoka shule ya upili ya Barani anasema kuwa kuna utofauti mkubwa kwenye makuzi ya mchezo huo tofauti na miaka ilopita.

Hata hivyo Huluma ametaja kuwa ukosefu wa vifaa vya kuchezea mchezo wa raga ndio changamoto kubwa inayowasibu kwa sasa akitolea mfano shule ya Maziwani ambayo imejitokeza kwa mashindano ya eneo bunge na kuona mpira wa raga kwa mara ya kwanza kabisa huku mashindano hayo yakiendelea.