Kipa nambari moja wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Cameroon Andree Onana anatarajiwa kukosa mechi ya kwanza ya Afcon wakati timu yake ya taifa itakuwa inacheza dhidi ya timu ya taifa ya Guinea.
Onana atakosa mechi hiyo baada ya kukubali kucheza mechi ya ligi katika klabu ya Manchester United jana dhidi ya Tottenham Hotspers kwenye ligi kuu Uingereza.
Taarifa za awali zilikuwa zasema kwamba huenda Onana angecheza mechi mbili ndani ya masaa 24 lakini hilo limeshindikana kwa mujibu wa taarifa ambazo zimeachiwa hivi punde, taarifa ambazo zimezua gumzo mitandaoni kwa sasa.
Michuano imeanza kwa kasi katika taifa ya Ivory Coast tangu siku ya jumamosi. Timu ya soka ya Misri imeponea chupuchupu kupata fedheha kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano hii dhidi ya Msumbiji uliomalizika kwa sare ya bao 2-2.
Mkwaju wa penati wa mshambuliaji Mohammed Salah mnamo dakika za majeruhi ndiyo uliwaokoa Misri na aibu ya kufungua pazia kwa kichapo kwenye mchezo huo wa kundi B.
Kwenye mchezo mwingine wa kundi B, timu ya soka ya Ghana ilikubali idhara kwa kucharazwa hadharani bao 2-1 na vijana wa Cape Verde. Kabla ya michezo ya kundi B, kulikuwa na mchezo wa kundi A kati ya Nigeria na Guinea ya Ikweta na ulimalizika kwa sare tasa ya bao 1-1.
Mechi za leo ni, Senegal vs Gambia 3-0, Cameron vs Guinea 1-1 kisha mwendo wa saa tano Algeria vs Angola.
Taifa la Ivory Coast ambao ni waandaaji wa mashindano haya pamoja na kwamba ni washindi mara mbili walishinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Guinea Bisau kwa mabao 2-0.
Mkufunzi wa Ivory Coast maarufu kama Ndovu ana matumaini ya kuandikisha matokeo bora msimu huu na kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza tangia mwaka wa 2015 timu hiyo chini ya uongozi wa nahodha Yaya Toure waliposhinda ubingwa.

