KENYA SHUJAA YATWAA UBINGWA DUBAI

Kenya Shujaa kikosi cha raga ya wachezaji saba kila upande ndio mabingwa wa mashindano ya msururu wa kombe la Dubai Challeger yalotamatika jana baada ya kuichapa Chile kichapo cha alama 12-5. Ni fainali ambayo ilimshuhudia  Patrick Odongo akifunga try mbili ambazo sasa zinawafanya vijana wa Kelvin Wambua kumaliza mashindano hayo katika nafasi ya kwanza.

Wakatihayo yakijiri kwa upande wa kinadada Kenya Lionesses walikubali kichapo cha alama 19-5 dhidi ya China katika finali na kuwafanya masimba jike hao kumaliza mashindano haya ya Dubai kwa alama 18 pekee.

Waziri wa michezo Ababu Namwamba ameungana na viongozi wengine wa Kenya kuwapongeza Shujaa pamoja na Lionesses kwa matokeo hayo mazuri.