MWENYEKITI WA KAMATI YA CDF MALINDI AWATAKA WENYEJI KUTOHOFU LOLOTE

Wakaazi wa eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wametakiwa kutokuwa na hofu kuhusiana na utendakazi wa kamati ya CDF, katika afisi ya mbunge wa Malindi, Amina Mnyazi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo Sammy Kazungu kamati hiyo inawakilisha kila jinsia na umri jambo ambalo amesema linasaidia kuhakikisha kila mmoja anajumuishwa katika kamati hiyo.

Akizungumza na wenyeji wa Malindi amesema licha ya kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, pia anajukumu la kuwasilisha matakwa ya wazee wa eneo hili, kwani aliteuliwa pia kuwakilisha wazee katika kamati hiyo.

Aidha, amesema kuwa kando na mbunge wa eneo hili kuwa na wawakilishi wake katika kamati hiyo pia uundwaji wa kamati hiyo ulizingatia sheria za kitaifa kuhusiana na masuala ya hazina ya CDF.