Gavana wa kaunti ya kwale Fatuma Achani amezindua rasmi ujenzi wa mradi wa mashini ya kuchuja maji katika hospitali ya rufaa ya Msambweni.
Mradi huo unatarajiwa kuzalisha zaidi ya lita 5000 za maji yanayochujwa kwa kila saa moja, maji ambayo yanatarajiwa kusaidia kuendesha shughuli za hospitali hiyo bila kukwama.
Vitengo ambavyo vinatarajiwa kunufaika na matumizi ya maji hayo ni kile cha upimaji magonjwa ya figo, upasuaji, utoaji damu, kitengo cha usafi wa hospitali pamoja na vitengo vingine.
Haya yanajiri wakati ambapo kumekua na tuhuma za ukosefu wa maji katika hospitali za msambweni na kinango ambapo Achani amepuuzilia mbali kauli hizo akisema hospitali za maeneo hayo zina maji ya kutosha.
Gavana Achani alikua ameandamana na wawakilishi wadi akiwemo Hanifa Mwajirani wa wadi ya Ramisi pamoja na mwakilishi wadi ya Pongwe kikoneni Mohammed Mwaduga.

