MUUNGANO WA WASIMAMIZI WA MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU WATOA LALAMA ZAO

Naibu katibu wa muungano wa wasimamizi wa madereva wa malori ya masafa marefu kaunti ya Mombasa Ahmed Omar amemtaka rais William Samoei Ruto kushugulikia matatizo wanayopitia madereva katika kutekeleza shughuli za kusafirisha mizigo kwenye maeneo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.
Akiongea na wanahabari Omar amesema kumekuwa na utovu wa usalama katika barabara kama ya Mombasa – Nairobi hali ambayo imesababisha wengi wao kuuliwa wanapokuwa safarini.
Wamemtaka kuweka mikakati thabiti ya kuboresha sekta hiyo ili kunusuru maisha ya madereva hao.
Ametaja pia mazingira duni ya kufanyia kazi akisema yanaathiri utendakazi wao.
Kauli yake imeungwa mkono na Mwenyekiti wa muungano wa madereva wa Malori ya masafa marefu kanda ya pwani Roman Waema ambaye amelalamikia misongamano ya magari mipakani ambayo anadai kuchangiwa na utepetevu wa maafisa walioko kwenye vituo vya kupima mizani ya magari hayo katika mipaka.
Kwa upande wake Lucy Kanyi mmoja wa maafisa wa muungano huo amemataka rais William Ruto kufanya vikao nao ili kupata suluhu la kudumu kutoaka na madhila ambayo wanayapitia kwenye sekta hiyo ya uchukuzi.