Waziri wa michezo hapa nchini Kipchumba Murkomen ametaja kuwa uchache wa michezo inayowasilishwa na Wakenya katika Olimpiki ndio jambo ambalo limechangia pakubwa kupitwa na mataifa mengine kwenye idadi ya medali mwaka huu.
Katika mashindano ya Olimpiki ya Paris Ufaransa mwaka huu Kenya ilisajili medali 11 pekee jambo ambalo Murkomen anahisi Kenya ingeviluna zaidi iwapo ingeshiriki kwenye michezo mingi.
Ameahidi kupambana kwenye kuboresha mashirikisho ili kuyafanya kuleta nidhamu na kuhusisha michezo zaidi kwenye Olimpiki ijayo.
Katika kusailiwa kwake kabla apewe wadhfa wa uwaziri Murkomen aliahidi kuwatimua maafisa washirikisho ambao hawajakuwa wakipiga kazi kwa wananchi akitolea mfano FKF ya rais wa sasa Nick mwendwa.

