wanaradha wa Kenya walioshiriki katika mashindano ya olimpiki ya mwaka huu jijini paris Ufaransa wamepokelewa na rais Willian Samoei ruto alfajiri ya leo kwenye dhifa maalum ya kiamsha kinywa mjini Eldoret.
Kati ya waliohudhuria hafla hiyo ni waziri wa michezo Kipchumba Murkomen na katibu wake Peter Tum miongoni mwa wanariadha wengine wakongwe.
Rais Ruto ametumia fursa hiyo kuwapongeza Team Kenya katika olimpiki za mwaka huu kwa kuonyesha ukakamavu mkubwa kwenye mashindano mbalimbali.
Amewashukuru kwa kupeperusha bebdera ya Kenya vilivyo jambo ambalo linazidi kuletea heshima taifa hili kwenye ngazi za kimataifa.
Kikosi cha Kenya kimerejea nchini na medali 11 na inaongoza Afrika kwa kushinda medali nyingi zaidi kwani bara zima la afrika lilivuna medali 38 nyingi zikiwa ni za Team Kenya.

