MURANGA SEAL YASISTIZA HUSSEIN AWEPO KWENYE KIKAO CHA FKF

Klabu ya Muranga Seal inayoshiriki ligi kuu ya FKF hapa nchini imeshikilia kwamba Husein Mohamed ataiwakilisha klabu hiyo katika mkutano mkubwa wa mwaka wa FKF jumamosi ijayo.

Husein Mohamed ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Extreme Sports shirika lilolotangaza kupeana udhamini kwa ligi ya kitaifa ya Super League alikuwa amefungiwa na shirikihso la soka la fkf kutoenda kwenye kikao hicho kikubwa cha mwaka tarehe 16.

Kulingana na katibu mkuu wa fkf Barry Otieno ni kuwa Mohamed alipigwa marufuku kwa kuwa yeye sio mwanachama halali wa fkf kivyovyote.

Kwa upande wa mmiliki wa klabu ya Muranga Seal Robert Macharia ni kuwa ni sharti Husein Mohamed aruhusiwe kuwa katika kikao hicho akiwakilisha Muranga Seal na hana nia ya kupeana nafasi ya uwakilishi kwa mtu mwengine kwa sasa.