Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa michezo katika klabu ya Liverpool kule Uingereza Michael Edwards amerejea rasmi sasa katika klabu hiyo baada ya kuondoka kwa muda.
Vishawishi vya wamiliki wa klabu hiyo vimezaa matunda ya kumrudisha gwiji huyo aliyehusika pakubwa katika kuunda kikosi cha Liverpool katika kipindi cha Jergen Klopp.
Alikuwa chanzo cha Liverpool kufanikiwa kuwasajili mastaa walioletea Liverpool ufanisi mkubwa Uingereza akiwemo Mo Salah, Sadio Mane, Virgil Van Dijk na wengineo.
Inasadikika kuwa huenda Fenway Sports Group ambao wanamiliki Liverpool wanataka kuanza mchakato wa kuwinda mkufunzi mpya pamoja na usajili utakao zidi kuisimamisha klabu hiyo ya Mersyside na Michael Edwards mwenye umri wa miaka 44 ndio tegemeo la kufanikisha mradi huo kwa sasa.

