Mkufunzi wa soka Rio Ngumbao anayeongoza timu ya kaunti ya kilifi katika mashindano ya KYISA yanayoendelea katika kaunti ya Tharaka Nithi amelalamikia maamuzi mabaya ya marefa akisema kwamba hayo ndiyo yanasababisha mpaka kufukia sasa hawaja sajili ushindi hata mmoja.
Rio akizungumza na Tama la Spoti kupitia njia ya simu anasema kwamba wachezaji wake wasiozidi umri wa miaka 23 wameanza kupoteza motisha wa kuendelea na mashindano hayo kutokana na maonevu ya wazi ambayo yalitokea jana uwanjani.
Mkufunzi Rio anasema kwamba kwa sasa nafasi za kufuzu kuingia katika hatua ya robo fainali ni hafifu sana kwani mpaka kufikia sasa wako na alama tatu katika chungu chao baada ya kupiga sare tatu.
Kwa upande wa kinadada katika mashindano hayo, kikosi kinachoongozwa na mkufunzi Fathime Tibu kimeingia katika hatua ya robo fainali baada ya kuitandika timu ya kaunti ya Nyandarua kichapo cha mabao 2-0.

