Mshirikishi wa utawala kanda ya Pwani Rodah Onyancha amedhibitisha kukamatwa kwa mchungaji wa kanisa la New Life Prayer Center, Ezekiel Odero katika eneo la Mavueni kaunti ya Kilifi Mapema hii leo.
Kulingana na mshirikishi huyo ni kuwa mchungaji huyo, alikamatwa kutokana na kuwepo kwa madai ya vifo vya baadhi ya waumini wake, ambavyo wanadai vimekuwa vikiripotiwa, katika baadhi ya makafani hapa kaunti ya Kilifi.
Akizungumza mda mfupi baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa dini, Onyancha amesema kuwa waumini wote waliokuwa katika kanisa hilo wametakiwa kutoka inje na nyumba ya hiyo ya ibada kufungwa kwa mda usiojulikana.
Ni hatua ambayo imeibua hisia mseto kutoka kwa wakaazi mbali mbali katika eneo hilo, ambao baadhi yao wameelezea kutoona sababu ya kiongozi huyo wa dini, kukamatwa na maafisa wa polisi.

