Klabu ya Paris Saint-Germain imemsimamisha mshambuliaji Lionel Messi kwa wiki mbili bila mshahara baada ya Nyota huyo raia ya Argentina kukwepa mazoezi ya klabu hiyo na kukwea pipa kuelekea Saudi Arabia bila idhini ya klabu.
Messi (35) alifunga safari hiyo baada kipigo cha PSG cha 3-1 nyumbani dhidi ya Lorient Jumapili iliyopita, ambapo alicheza dakika zote 90. Inaelezwa mshindi huyo mara 7 wa Ballon d’or aliomba ruhusa ya kufanya safari hiyo ya kibiashara lakini alikataliwa.
Messi ana majukumu kama balozi wa utalii wa Saudi Arabia, na alisafiri kwenda katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati kwa shughuli za kibiashara.
Messi hataweza kucheza/kufanya mazoezi wala kulipwa kwa wiki mbili zijazo ikiwa hakutakuwa na mabadiliko kwenye adhabu hiyo iliyoamuliwa na PSG.

