Refa wa Kenya wa kike Mary Njoroge ni kati ya kikosi cha marefa kitakachotumika katika mashindano ya kombe la dunia la kinadada mwaka huu yatakayoanza rasmi mwezi huu wa Julai tarehe 20 mwaka huu 2023.
Mashindano hayo yatakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja yanaandaliwa na taifa la Australia pamoja na taifa la New Zealand.
Mary Njoroge anaamini kwamba nafasi hiyo ya kipekee itawapa motisha wachezaji au hata waamuzi wa kike kujiunga na michezo katika ngazi kubwa na kutafuta mafanikio kupitia vipawa vyao.
Refa huyu wa kike amekuwa akihusika katika mashindano makubwa yakiwemo kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar pamoja na mengine makubwa kama vile Tokyo Olympics mwaka 2020.

