ANCELOTTTI KUWA MKUFUNZI MPYA WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL

Mkufunzi wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti atakuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya brazil kuanzia mwaka ujao.

Hii ni kulingana na rais wa shirikisho la soka la brazil Ednaldo Rodriguez aliyesema kuwa wako mbioni kutafuta huduma za kimkataba na Ancelotti.

Kwa sasa anayeongoza Samba Boys ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia  kama mkufunzi wa muda ni kocha wa klabu ya Fluminence mwite Fernando Dinis.

Carlo Anceloti ambaye mkataba wake na Madrid unatamatika mwishoni mwa msimu ujao atakuwa anachukua jukumu la kuwaongoza samba boys kwenye mashindano ya Copa Amerika mwaka 2024 kama mkufunzi wa kwanza wa kigeni kuwahi ongoza timu ya taifa ya Brazil tangu mwaka 1965.