MAJERAHA YA AFCON YA MO SALAH KUTOBIWA LIVERPOOL

Mkufunzi wa klabu ya Liverpool Jergen Klopp amethibitisha kuwa Mohamed Salah atalazimika kurejea katika viunga vya Mersyside huko Liverpool kutibiwa na madaktari wa klabu hiyo baada ya kupata jeraha la misuli kwenye mechi ya afcon ambapo Salah alikuwa anawakilisha misri dhidi ya Ghana.

Kulingana na Klopp ni kuwa iwapo Mo Salah atapona kwa wakati basi huenda akarejea katika mashindano ya kombe la Afcon mashindao yanayoendelea huko Ivory Coast.

Shirikisho la soka la Misri limethibitisha kuwa limewasilisana na uongozi wa Liverpool kuhusiana na jeraha la Salah na huenda akasafiri baada ya mechi ya leo dhidi ya timu ya taifa ya Cape Verde mwendo wa saa tano usiku.

Mo Salah ni mwanafainali ya Afcon makala yalopita ambapo alipoteza kombe hilo mikononi mwa Senegal kupitia matuta. Kwa sasa anaongoza kwa mabao katika ligi kuu ya Uingereza akiwa amefunga mabao 14 na kutoa assists 8