KOCHA WA TAIFA STARS AFUNGIWA NA CAF

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limempa adhabu ya kumfungia mechi nane aliyekuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya soka Tanzania Taifa Stars mwite Adel Amrouche kutokana na matamshi yake ya kupeana taarifa za uongo wiki jana kabla ya mechi dhidi ya timu ya taifa ya Morocco.

Mkufunzi Adel alikuwa amesema kwamba shrikisho la soka la Morocco makusudi linapanga ni marefa wapi lakini pia muda wao wa kucheza mechi, jambo ambalo limekanushwa na si shirikisho la soka la tamzania maarufu kama TFF pamoja na CAF.

Kutokana na hilo shirikisho la soka TFF lilitangaza kumfuta kazi kocha huyo na kumpa ukocha wa muda Hemed Suleiman kongoza Taifa stars kwenye mechi zilizosalia ikiwemo mechi ya jana ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Chipolopolo  ya Zambia.

Kufikia sasa Tanzania imecheza mechi mbili Afcon msimu huu huko Ivory Coast na imesajili sare moja 1-1 dhidi ya Zambia na kupigwa mara moja na timu ya taifa ya Morocco kichapo cha 3-0