MAGAVANA KANDA YA PWANI WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Wito umetolewa kwa magavana kaunti za pwani kushirikiana na kuwa kitu kimoja kwa minajili ya kuboresha maendeleo ya ukanda huu wa pwani.
Ni wito uliotolewa kwenye kongamano la jumuiya ya kaunti za pwani linalofanyika mjini Hola kaunti ya Tana river ambapo viongozi wamesema kuwa ukanda huu pwani una uwezo wa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 za ushuru kila mwaka.
Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdallah Timammy amesema kuwa serikali ya kitaifa haipaswi kuingilia masuala ya uchumi wa baharini ila iwachie kaunti hasa za pwani zishughulike kikamilifu kwenye masuala hayo.
Naye gavana wa Taita Taveta Andrew Mwadime, gavana wa Tanariver Dhadho Gadhae Godhana na gavana wa Kilifi Gedion Maitha Mung’aro wamesisitiza haja ya magavana wa kaunti za pwani kushirikiana kuimarisha kaunti hizi kiuchumi pasi na kuzingatia misimamo ya kisiasa.