Sehemu nyingi nchini zinapoendelea kukabiliwa na makali ya njaa na ukame serikali ya kaunti ya Lamu ikishirikiana na serekali kuu zimeanzisha mpango wa kupeana na chakula cha msaada kwa familia elfu kumi na mbili katika kaunti ya Lamu.
Kutokana na hali hiyo, Vijiji ambavyo vinavyolengwa ni pamoja na Bargoni, Basuba, Kiunga, Kiongwe, Lumshi, maisha Masha, Jipendeni na Witu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa chakula hicho eneo la Mswakini wadi ya Hindi gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy amesema wamechagua sehemu kadhaa zilizoathirika zaidi na ukame ili kuwapa chakula hicho cha msaada.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa kaunti ya Lamu Charlse Kitheka amewataka wenyeji ambao ni walengwa kuwa na subira kwani kila mmoja atapokea chakula hicho cha msaada huku mwakilishi wa wadi ya Hindi James Njaaga akiwataka wenyeji kutumia tingatinga ambazo zimetolewa na serikali ya kaunti hiyo kwa ajili ya shughuli za kilimo.
SERIKALI YA LAMU NA YA KITAIFA ZASHIRIKIANA KUPEANA CHAKULA CHA MSAADA

